MAGONJWA KWA VIFARANGA WA KIENYEJI
Magonjwa ya Vifaranga vya Kuku wa Kienyeji ni changamoto kubwa kwenye ufugaji wa kuku ambayo huwakatisha tamaa Wafugaji wengi kwa sababu ya vifo vingi hasa kipindi cha uleaji wa vifaranga vya kukuwakienyeji. Magonjwa yamegawanyika katika makundi mbalimbali kulingana na wadudu wanaosababisha magonjwa hayo. Kuna magonjwa yanayo sababishwa na virusi, magonjwa yanayo sababishwa na bakteria, magonjwa yanayo sababishwa na protozoa, magonjwa ya upungufu wa lishe na magonjwa yanayosababishwa na wadudu (minyoo, viroboto na utitiri). Bakteria wanaosababisha magonjwa ya vifaranga vya kuku wa kienyeji hupatikana kwenye miili ya kuku wagonjwa, utumbo, makamasi, na vinyesi vyao. Aidha, katika mazingira machafu na vyakula, maji, hewa, na vifaa vya kazi vilivyo chafuliwa. Mazingira yenye unyevunyevu na joto ni vichocheo vya kuzaliana na kusambaa kwa hao bakteria. Magonjwa ambayo hasa huwapata vifaranga mara kwa mara 1. Typhoid 2. Kipindupindu 3. Coccidiosis...