NDUI YA KUKU(FOWL POX)
Ndui ni ugonjwa unaosababishwa na virusi ambavyo hushambulia zaidi kuku, jamii ya bata na aina nyingi ya ndege pori. Kuku na ndege wa umri tofauti wote huweza kushambuliwa na sehemu zinazoathirika zaidi ni zile zisizo na manyoya. Virusi vinaweza kuishi katika mazingira kwa muda mrefu.
Jinsi Ugonjwa Unavyoenea.
-Chanzo cha maambukizi ni vifaa/vyombo vya shambani vilivyochafuliwa na kinyesi cha kuku wagonjwa na wenye vimelea.
-Maambukizi pia kuenea kupitia wadudu wanaouma kama chawa, kupe, nzi weusi na mbu.
-Maambukizi pia kuenea kupitia majeraha wanayoyapata kuku wanapopigana na kukwaruzana au kugusana Maambukizi kupitia mfumo wa hewa na chakula.
Dalili
Kuku aliyevimba macho
Ugonjwa unapoathiri ngozi hutokea vipele vikubwa vya rangi ya kijivu au kahawia kwenye upanga, undu, macho na mdomoni au sehemu zisizo na manyoya. Ugonjwa unapoathiri sehemu laini za mwili, mabaka madogo meupe hutokea kwenye kona za mdomo, kuzunguka ulimi, ndani ya mdomo na kwenye koo. Malengelenge kwenye kishungi na kope za macho na sehemu zisizo na manyoya.
Namna ya kuzuia ugonjwa na tiba
-Ni ugonjwa unaosababishwa na virusi hivyo hauna chanjo.
-Kuchanja kuku wote wakiwa na wiki ya 4 hadi ya 5 hasa siku 30. kwa kutumia chanjo ya fowlpox au tatu moja
NB: njia hii ina hitaji mtaalam au daktali wa mifugo-Watenge kuku wote walioambukizwa na wapewe antibiotic kama OTC plus au salfa pamoja na kusfisha vidonda kwa maji ya chumvi
Imeandaliwa na
jedidiah mattaba
MTAALAMU WA KUKU
0621627094




Maoni
Chapisha Maoni