SABABU ZA KUKU KULA MAYAI

 


Kuku hula mayai kwa sababu nyingi sana ambazo zingine au zote zinaweza kuzuilika,
1.Tabia yao tu- Hapa utakuta ndo uzao wao wanatabia ya kula mayai hivyo kuku hufanya muendelezo wa kula mayai,

2.Kuto kupata chakula cha kutosha- Hii ni moja ya sababu kubwa kabisa inayo pelekea kuku kula mayai.

3.Kukosa madini joto- Hii inaweza kuwa ndo sababu kuu ya kwa nini kuku wanakula mayai, kuku wakikosa madini joto ni lazima wale mayai na hata kulana wao wenyewe,
.
4.Lishe mbaya chakula unacho wapatia huja changanya na
 madini yeyote

5.Nafasi ndogo ambayo ita sababisha msongamano na kupelekea kudonoana  au kula mayai.

6.Kukosa shughuli kama za kuparua au kula chakula

7.Ukoo/aina au asili ya kuku anayo tokea


NAMNA YA KUZUIA KUKU KUDONOANA AU KULA MAYAI
1.Chakula cha kutosha ni muhimu sana, ili kuwafanya wasitake kula mayai ili kushiba.

2.Maji yakusanywe mara tu anapo taga na usiyaache muda mrefu bandani.

3.Sehemu ya kutagia iwe na giza la kutosha ili kufanya kuku ashindwe kuona yai alilo taga.

4.Madini joto ni muhimu sana.

5.Kuku wenye tabia za kula mayai unaweza chinja au kuuza.

6.Kuweka idadi ya kuku inayolingana na sehem ulionayo.

7.Usizidishe mwanga.

8.Banda liwe safi.

9.Weka vyombo vya kutosha.

10.Wape lishe bora.

11.Wape kuku shughuli kwa kuwawekea bembea na sehemu ya uwazi kwa ajili ya mazoezi.

12.Kata midomo ya juu kwa kuku ambaye amesha zoea kula mayai.

13.Epuka ukoo wenye tabia hizo.

Imeandaliwa na

*  jedidiah mattaba

                  MTAALAMU WA KUKU

                 0621627094

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

MAGONJWA KWA VIFARANGA WA KIENYEJI

MDONDO/KIDERI(NEWCASTLE DISEASE)

MAFUA MAKALI (INFECTIOUS CORYZA)