SABABU ZA KUKU KULA MAYAI
Kuku hula mayai kwa sababu nyingi sana ambazo zingine au zote zinaweza kuzuilika, 1.Tabia yao tu- Hapa utakuta ndo uzao wao wanatabia ya kula mayai hivyo kuku hufanya muendelezo wa kula mayai, 2.Kuto kupata chakula cha kutosha- Hii ni moja ya sababu kubwa kabisa inayo pelekea kuku kula mayai. 3.Kukosa madini joto- Hii inaweza kuwa ndo sababu kuu ya kwa nini kuku wanakula mayai, kuku wakikosa madini joto ni lazima wale mayai na hata kulana wao wenyewe, . 4.Lishe mbaya chakula unacho wapatia huja changanya na madini yeyote 5.Nafasi ndogo ambayo ita sababisha msongamano na kupelekea kudonoana au kula mayai. 6.Kukosa shughuli kama za kuparua au kula chakula 7.Ukoo/aina au asili ya kuku anayo tokea NAMNA YA KUZUIA KUKU KUDONOANA AU KULA MAYAI 1.Chakula cha kutosha ni muhimu sana, ili kuwafanya wasitake kula mayai ili kushiba. 2.Maji yakusanywe mara tu anapo taga na usiyaache muda mrefu bandani. 3.Sehemu ya kutagia iwe na giza la kutosha ili kufanya kuku ashindwe kuona yai ...